ZIJUE ISHARA ZA MIWASHO MWILINI MWAKO KINYOTA:

Utakubaliana na mimi kwamba hakuna kiumbe hai
ambacho hakijawahi kuwashwa, tukianzia kwetu sisi
wanadamu hadi wanyama, ukiachilia mbali na
miwasho ya mtu anayesumbiliwa na maradhi au
kunguni, ipo yenye kutoa ishara mbalimbali kinyota
kama vile :
(1). KIGANJA CHA KULIA : Hii ni ishara ya kupata
pesa au kufanikiwa katika jambo fulani linalohusu
masuala ya kipato.
(2). KIGANJA CHA KUSHOTO : Wanajimu wengi wa
masuala ya nyota wanaeleza kama ishara ya
kupoteza, huenda ikawa fedha au kitu chenye
thamani.
(3). UKIWASHWA TUMBONI : Tegemea kupata
mualiko wa shughuli yeyote inaweza ikawa sherehe,
mahafali au tafrija.
(4). KUWASHWA MAKALIONI : Unaweza ukapata
suluhu ya jambo lako , kutatuliwa shida zako au
kuteulia kuwa msuluhishi.
(5). GOTI KUWASHA : Utapokea habari za kizushu,
uongo na umbea.
(6). PAJA KUWASHA : Huenda ukahama sehemu
ulipo au ukahamishwa kikazi.
(7). JICHO LA KULIA KUCHEZA : Utapata furaha,
mipango yako kufanikiwa na kufunguka kwa ridhiki
na mengine mazuri
(8). JICHO LA KUSHOTO KUCHEZA :
Kupalanganyika kwa mambo yako, nuksi, balaa na
mikosi kukuandama kama umezaliwa nayo.
(9). KUWASHWA NJE YA PUA : Kero, machukizo na
mauzi ya kila aina.
(10). KIFUNDO CHA MGUU WA KULIA : Utapata
pesa na wadeni wako kukulipa.
(11). KIFUNDO CHA MGUU WA KUSHOTO : Kudaiwa
na wanaokudai kukufuata au kukutafuta.
(12). KICHWA KUWASHA : Kupata pesa kiurahisi na
biashara za haraka haraka zenye faidi kubwa.
.TUNZA HII SIKU UKIWASHWA UNAKUJA KUSOMA TU USINGOJE MPAKA NIJE NIKUJIBU

+255743127450

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *