Kujiuzulu kwa Borne kumekuja wakati ambapo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitarajiwa kufanya mabadiliko ya timu yake ya viongozi wa juu kabla ya chaguzi za Ulaya baadae mwaka huu.
Rais Macron amesema katika uongozi wake Waziri Borne alionyesha dhamira, kujitolea na ujasiri mkuu.
Borne ambaye alishika wadhifa huo Mei 2022 ataendelea nao hadi Waziri Mkuu mpya atakapotajwa.
Alikuwa Waziri Mkuu wa pili Mwanamke nchini humo, akitanguliwa na Edith Cresson aliyeshika nafasi hiyo mwaka 1991 hadi 1992.