UKIWA NA TABIA HIZI KAMWE HUTAKUJA KUPIGA HATUA KIMAISHA.

  1. TABIA YA KUSHINDANA (COMPETITION LIFE).
    🎯Kama wewe ni mtu ambaye unapenda kushindana basi sahau kupiga hatua kimaisha. Sahau kufikia ndoto zako, sahau kuwa mtu mkuu, sahau kuwa mtu uliyefanikiwa.

Kama unaishi maisha ya kununua vitu kisa mtu mwingine kanunua hutakuja kutoboa…

Kama unaishi maisha ya kumpeleka mtoto katika shule za gharama kisa fulani kafanya hivyo kupiga hatua sahau…

Kama unaishi maisha ya kwenda kustarehe sehemu za gharama kisa fulani kaenda hutakuja kutoboa

Sahau….

  1. TABIA YA KUKOSA UVUMILIVU
    🎯 Uvumilivu ni tunda la Roho Mtakatifu, uvumilivu ni sifa ya mwenyezi Mungu ambapo anapenda na wanadamu wawe na moyo wa uvumilivu…

Sasa ukikosa uvumilivu sahau kufikia hatima yako, sahau kuzipata ahadi za Mungu, sahau kufanikiwa…

Kama unaishi maisha ya kuishia njiani kwenye biashara, karama au kitu chochote ambacho unakifanya basi sahau kutoboa…

Kama unaishi maisha ya kuacha kufanya kitu kisa kuna ugumu basi kutoboa sahau…

Huwezi kufanikiwa kama huna uvumilivu….

  1. TABIA YA KUYACHUKIA MAARIFA
    🎯Usipopenda maarifa wewe tayari ni mtu mfu. Maarifa ni mlango wa kufanikiwa ikiwa na maana usipokuwa nayo basi hutaweza kutoboa kimaisha.

Kama vitabu unaviona ni mama mkwe kutoboa sahau…

Kama unaona kulipia kozi, seminar ni upuuzi au kukosa muda basi sahau kutoboa kimaisha…

Kama ma group ya mafundisho, unaona ni ujinga basi kutoboa sahau…

“Kila ayachukiaye maarifa hutafuta kifo”.

Je wewe unapenda maarifa?

Ina maana ukitaka kutoboa hakikisha…

(a) Unaacha maisha ya kushindana

(b) Unakuwa ni mtu ambaye una uvumilivu

(c) Unakuwa ni mtu ambaye unapenda maarifa sana….

Otherwise nikutakie heri ya mwaka mpya kwa Mara nyingine Tena…

Nakupenda ❤️

Like, Comment, share and Save

MwlHekimaMwasile