Rwanda imesema imesikitishwa na hatua ya Burundi kuifunga mipaka yake ikieleza kuwa watakaoumia ni raia ambao wamekuwa wakifanya biashara na shughuli mbali mbali kupitia mpaka wa Rugombo mkoani Cibitoke na Ngozi licha ya kutofunga njia ya anga.
Pia serikali imebainisha kuwafukuza raia wote wa Rwanda waliopo katika ardhi ya Burundi huku ikielezea kuwa ni miongoni mwa wapelelezi wa serikali ya Rais Paul Kagame.
Hii si mara ya kwanza Burundi kufanya hivyo ambapo mwaka wa 2015 iliifunga mipaka yake na Rwanda baada ya kuishutumu kuwaficha washukiwa wa jaribio la mapinduzi dhidi ya hayati Rais Pierre Nkurunziza ambalo lilifeli baadae.
Burundi imesema imefunga mpaka wake na Rwanda kuanzia tarehe 11 Januari ,2024, ikiwa ni wiki mbili sasa baada ya kulituhumu taifa hilo jirani kuwaunga mkono waasi waliofanya mashambulizi nchini humo na kuhatarisha usalama wa nchi.