RAIS PUTIN KUFANYA ZIARA BURUNDI.

Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajia kufanya ziara barani Afrika mwaka huu wa 2024, Burundi na Equatorial Guinea ikiwa ni miongoni mwa nchi atakazofanya ziara yake.

Hata hivyo Ikulu ya Urusi, Kremlin bado haijaweka wazi tarehe ya ziara yake kwani muhula wa Rais huyo unatarajia kumalizika Mei,2024.

Hakuna ziara za kutembelea nchi zisizo rafiki ambayo imepangwa kufanyika.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Urusi siku ya Ijumaa ilisajili wagombea wawili wa kwanza ambao watashindana na Rais Vladimir Putin katika uchaguzi wa Machi 2024 ambao Putin ana uhakika wa kushinda.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *