NYUMBA YA KATUMBI YAZUNGUKWA NA WALINDA USALAMA

Mkuu wa mkoa wa Katanga nchini Jamhuri ya Kimokrasia ya Congo amewaamuru walinda usalama kuondoka nyumbani kwa aliyekuwa Mgombea wa kiti cha Urais Moise Katumbi.

Kwa mjibu wa Jacques Kyabula amesema kuwa ilikuwa ni kinyume na sheria kwa walinda usalama kuizingira nyumba ya Mwanasiasa huyo ambaye alikuwa ameamriwa kutotoka ndani ya nyumba.

Katumbi alikamata nafasi ya pili katika uchaguzi wa Urais kwa kupata asilimia 18 ya kura zilizopigwa huku Felix Tshiskedi akitangazwa kuwa mshindi wa Urais kwa kupata asilimia 73.

Katika tangazo lililotolewa Jumapili wiki iliyopita aliwataka Umoja wa Mataifa kutokubali ushindi wa Bw.Felix kwa madai ya kughubikwa na wizi wa kura.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *