Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai wetu ni afya, unene na kutojua kujiangalia vyema.
1-ULAJI
Ipo mifumo miwili ya kula.
Chakula unachokula
Unavyokula.
-Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo.
Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache.
Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka.
USHAURI:
Asubuhi: Kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi)
Vimengenya chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mf: vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomengenya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga.
Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine.
Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu.
-Mseto wa vyakula pia ni muhimu.
Vyakula vyenye uchachu (acid) na vile vinavyomumunyuka haraka (alkaline) havitakiwi viliwe pamoja. (Ili vifyonzwe vizuri)
Mfano ni matunda. Matunda chachu kama machungwa, mananasi na maembe yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi: ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti, wa kumengenywa.
Nyama nyeupe (ndege na samaki) tofauti na nyama nyekundu (ngombe, kondoo, nk) ziliwe tofauti.
Chakula unachokula
Waafrika hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.
Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara lolote duniani lakini sisi tunakufa mapema na kwa utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi kame.
Ulaya nzima imejazana mboga mboga zinazoagizwa toka Afrika. Kenya na Tanzania zinauza mboga za maharagwe mabichi (green beans), matunda toka Afrika Kusini na Ivory Coast; nk.
Waafrika tunapenda kujaza matumbo. Unene umekithiri hata wale walio matajiri waliosoma bado wanakufa kwa kisukari shauri ya kutokula mboga mbichi.
Ulaji wa mboga mbichi ni upi?
Ni mathalani ulaji wa kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu, giligilani na karote.
Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk).
Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana katika unene.
2-UNYWAJI MAJI
Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake.
Wanaokunywa maji zaidi ni wacheza michezo.
Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi na gesi za kisasa kama Red Bull) zilizojaa gesi inayoleta vidonda tumboni; na chai. Kuliko maji.
Na maji haya hutakiwa dakika 10-20 kabla ya chakula au nusu saa kuendelea baada ya chakula.
Unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvu za chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmengenyo wa chakula (digestion).
Chakula kisipomengenywa vizuri kinaketi tu tumboni. Matokeo wengi wetu tuna matumbo makubwa.
Kama hufanyi mazoezi lile tumbo linakwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo linaleta adha ya kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo.
3-SUALA LA UMENGENYAJI
Chakula huanza kumengenywa au kusagwa mdomoni.
Mate yako mdomoni ni chanzo cha uchambuaji chakula.
Unapobugia chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha mambo mawili.
Chakula kutochambuliwa vizuri,
Chakula kwenda kukaa tu tumboni, au kama kikipita hakisaidii lolote mwilini.
Utafunaji wa taratibu husaidia umengenyaji.
Chakula kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini.
Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo Hydrochloric) inayokibadilisha tayari kupelekwa utumbo mkubwa, kupitia kongosho.
Kule uchafu utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na utumbo mdogo kuelekea katika uwengu, moyo. Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba hubakishwa katika ini.
Sasa kama usipotafuna vizuri, ukila huku unakunywa sana maji au vinywaji vingine chakula hakimengenywi vizuri.
Ndiyo maana unawaona watu wengine wanakula sana lakini hawana afya.
Wanaugua ovyo ovyo, wanatoka jasho ovyo, wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa, wanavimbiwa, wanakaa siku nyingi bila kwenda choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa mara moja au mbili kwa siku) nk.
4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA
Mafuta ni suala muhimu sana mwilini.
Ila ulaji wake shurti uwe wa mpangilio.
Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya nguvu, yaani wanga (ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk), ujenzi yaani protini (mboga na nyama), madini (mbegu mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na vitamini (matunda, maziwa, mayai, nk).
Tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma (nyama nyekundu) protini, nguvu na mafuta.
Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri shauri huganda.
Ni vizuri nyama ya kuku na samaki ambayo hula na ngozi. Mafuta ya samaki ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na kinga maradhi mwilini.
Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku.
Kama huwezi kukaa bila nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.
USHAURI- Kula mbegu mbegu za korosho, karanga au mlozi (zikiwa mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku.
Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.
5-MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO
Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.
Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi.
Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Kama kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.
FAIDA-Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu.
Mazoezi yanayosaidia- kutembea kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha, kuendesha baisikel mwendo mrefu n.k
Mazoezi angalau mara mbili tatu kwa juma.
Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene lkn pia kurefusha maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk.
6-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI
Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha.
Kisayansi vyakula vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo Sodium. Sodium inachangia sana kufupisha maisha.
Huifanya mishipa ya damu ichoke; Mf. ni kama bomba lolote la maji yenye chumvi ukilitazama baadaye hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku.
Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni muhimu.
Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa chumvi na sukari.
7-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI KUHUSIANA NA AFYA
-Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza mwaka jana kwamba utapunguza ugonjwa wa moyo (ambao husababishwa na unene , wasiwasi na purukshani) kwa 42% kama utakula matunda na mboga za majani peke yake kila siku mbali na milo yetu yakawaida kawaida.
-Utafiti uliofanywa na wanasayansi chuo kikuu cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010 kuhusu faida za kuogelea.
Zoezi la kuogelea linapunguza unene zaidi ya kukimbia au kutembea kwa vile huchanganya mazoezi makali na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo kwa 50%.(hupunguza mafuta mwilini)
8-KUFUNGA
Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na Waislamu (mwezi Ramadhani) au Wakristo. Ufungaji huo una masharti mengine ya kidini tofauti na haya ya kiafya.
Ufungaji ni nini?
Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na kujisafisha.
Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini vinafanya kazi.
Faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo na kusafisha uchafu mwilini.
Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.
1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea
Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio.
Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA unavyofungua.
Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu. Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika.
Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo huu.
Maana lengo lake ni kusafisha mwili.
9-USINGAJI
Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya kupunguza unene.
Ikiwa unaangalia namna unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara moja au mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri.
Nini faida ya usingaji? Kusinga husaidia ngozi, mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na taswira yako mwanadamu.
Wengi wetu tunaposikia neno kusinga tunafikiria usingaji wa mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji wa mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia.
Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na kuungalia mwili wako kama nyumba au hekalu lako.
Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi, tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili yetu kiundani inaoza taratibu
See Insights and Ads
Like
Comment
Share