MTOTO WA RAIS WA MAREKANI HUNTER BIDEN ASHITAKIWA KWA MAKOSA TISA YA KUKWEPA KULIPA KODI.

MTOTO WA RAIS WA MAREKANI HUNTER BIDEN ASHITAKIWA KWA MAKOSA TISA YA KUKWEPA KULIPA KODI.

Mtotowa Rais, waMarekani Joe Biden, Hunter Biden ameshtakiwa kwa makosa tisa ya uhalifu unaohusiana na kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha dola milioni 1.4 anayodaiwa na Serikali.

Kulingana na hati zilizowasilishwa katika mahakama ya Los Angeles, Biden anashutumiwa kushindwa kuwasilisha na kulipakodi, kukwepa kutoata thmini ya kodi, nakurejesha kodi ya uongo au yaulaghai kati ya mwaka 2016 na 2019 huku akitumia mamilioni y adola kwa starehe.

Biden anakabiliwa na adhabu ya hukumu ya zaidi ya miaka 17 jela iwapoatapatika na hatia

Mweziuliopita, Hunter Biden alikana mashtaka matatu yanayohusiana na silaha baada ya jaji kukataa kutiasaini makubaliano ya rufaa ambayo yange epuka kesi ndefu za kisheria.

Kesi hii ya jinai huenda ikatia doa mchakato wa Rais Biden wa kuchaguliwa tena kuiongoza Nchi hiyo 2024 huku kukiwa na madai ya Republican kwamba mtoto wake alitumia vibaya nafasi ya babake kutengeneza mamilioni ya dola kupitia mikataba ya biashara na kazi ya ushauri katika nchi za kigeni zikiwemo Ukraine, China na Romania.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *