MAREKANI YASIKITISHWA NA MATAMSHI YA RAIS NDAYISHIMIYE

Marekani imeonyesha wasi wasi kuhusu matamshi ya hivi karibuni ya Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi kuwa wanapaswa kupeleka kwenye viwanja vya michezo na kuuawa kwa kutumia mawe watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi ya moja.

Marekani imefahamisha kuwa kauli hiyo itasababisha ukiukwaji wa haki za binadamu na watu hao kuishi kwa hofu katika nchi hiyo ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller ameitaka Burundi kuheshimu haki za binadamu bila ubaguzi wa mtu yeyote.

“Kuheshimu haki za binadamu kutasababisha nchi kuendelea na maisha ya watu hao kuwa mazuri” amesema.

Hata hivyo Rais Evariste Ndayishimiye hivi karibuni alifahamisha kuwa hakuna haja ya kupata au kupokea mikopo kutoka kwa watu wenye nia kama hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *