MAMBO 20 AMBAYO WANAWAKE WENYE AKILI TIMAMU HAWAFANYI KATIKA MAHUSIANO…..
Kile unachofanya au kutofanya kama mwanawake katika uhusiano huathiri sana mafanikio yako katika eneo la maisha ya urafiki au uchumba kabla ya ndoa..
Kama mwanamke mwenye utimamu wa Akili, Kabla ya kuingia katika maisha ya Ndoa kuna mambo unapaswa kufanya ili kuwa na uzoefu mzuri wa maisha yako ya stage ya urafiki au uchumba na kuna mambo ambayo hupaswi kufanya kabisa.
Je, ni mambo gani 20 ambayo wanawake wenye akili hawafanyi katika uhusiano wa kimapenzi?.
#1.. Hawaombi kupendwa.
Wanawake wenye akili wanaelewa kuwa uhusiano wenye afya unaimarishwa kwa nguvu za pande zote mbili, Hivyo huwa hawaombi kupendwa. Pia, wanajua thamani yao waliyobeba pasipo kujali madhaifu yao.
Hawajisikii kuwa hawastahili kupendwa na mwanamume, bila kujali umri wao, maisha ya zamani au hali ya kijamii na kiuchumi.Hawasiti kumwonyesha mwanaume mlango wa kutokea ikiwa anatishia kuwaacha, Hawamsihi abaki katika maisha yao kwa sababu wanaelewa kuwa hawafanyi wema ili waendelee kuwa katika mahusiano.
Wanawake wenye akili wanajua kuwa mwanaume unayempata kwa kumuomba atadumishwa kwako kwa kumuomba kila siku..
#2. Hawapigani na wanawake wengine kwa ajili ya mwanaume.
Hutawahi kumuona mwanamke mwenye akili timamu akipigana na mwanamke mwingine kwa ajili ya mwanaume. Mwanamke mwenye akili tukio hili kwake huwa jambo la aibu sana!
Mwanamke mwenye akili huamini kuwa;-
Mwanamke yeyote unayemkamata na mwanaume wako sio mkosaji.Kwa hakika, nyote wawili ni wahasiriwa wa mwanamume asiye mwaminifu. Hivyo hamna haja ya kugombana nyie wenyewe kwa ajili ya mwanaume.
#3..Hawaingii kwenye uhusiano kutafuta thamani.
Japo kuwa jamii inavutiwa kila wakati kuona ni mwanamke gani amechumbiwa, Wanawake wenye akili huwa hawaruhusu thamani yao kuamuliwa na wanaume au la. Hawafanyi maamuzi ya kuolewa kuifurahisha Jamii, wanafanya maamuzi ya kuingia katika ndoa kwa kuilinda thamani yao.
#4. Hawaruhusu mahusiano yawe kikwazo cha kutimiza ndoto zao.
Wanawake wenye akili huwa na maono ya maisha yao, kamwe hawakubali mahusiano yawe giza katika utimizaji wa maono yao, wapo tayari kuingia katika mahusiano na mwanaume anayeshimu maono yao.
Aina hii ya wanawake katika mahusiano huendana na wanaume wanaowapa changamoto za mafanikio.Wanaume wanaowahimiza na kuwasukuma kufikia ndoto za maisha yao .
Ana hii ya wanawake huamini kuwa maana ya maisha yao, utimizaji wa maono au ndoto za maisha yao ni zaidi ya maisha ya mahusiano.
#5 Mahusiano hawayafanyi kuwa ndio kusudi la maisha yao pekee.
Wanawake wenye akili huamini kuwa, maisha yao si kwa ajili ya mahusiano pekee yake. Aina hii ya wanawake hawaishi mahusiano, wanaishi maisha yao.
Hueleza kuwa maisha yao huwa na furaha zaidi wanapoambatana na mwanaume anayetambua kuwa wana fursa wao pia ya kuishi maisha yao, nasio mwanaume anayewachukulia kuwa maisha yao ni kwa ajili ya mahusiano pekee yake.
#6 Hawajifanyi kuwa sio wao ili kumfurahisha mwanaume.
Wanawake wenye akili hawajifanyi kupenda wasichopenda ili kumfanya mwanaume awapende. Hawaamini katika kufanya kitu ambacho hawana raha nacho ili kumfurahisha Mwanaume.
#7 Hawaachi ndoto zao ili kuwa na mwanaume.
Wanawake wenye wenye akili hawaachi ndoto zao kwa sababu yoyote ile. Wanaelewa kuwa; utimizaji wa ndoto zao huwapa utambulisho katika maisha yao. Mahusiano yasiyounga mkono ndoto zao hayana nafasi kwao.
#8 Hawapuuzi familia zao na marafiki zao kwa sababu ya mwanaume.
Wanawake wengi wanaoingia katika mahusiano uhusiano wao unakuwa kitovu cha maisha yao hali inayowapelekea kupuuza kila uhusiano mwingine katika maisha yao, Siku uhusiano wao utapoharibika wanakumbuka familia zao na marafiki zao.
Kwa wanawake wenye akili jambi hili ni tofauti kwao, wanaelewa kuwa: uhusiano wa kimapenzi sio uhusiano pekee wanaohitaji katika maisha yao, mahusiano mengine pia ni muhimu pia kuyadumisha katika mahusiano yao.
#9 Hawapotezi thamani ya mwili wao kwa ajili ya mahusiano.
Wanawake wenye akili ni waangalifu sana katika kujitunza wasipoteze
thamani ya mwili wao. Hawajirahisi kwa kila mwanaume kumvulia nguo aujue mwili wao.
#10 Hawapuuzi bendera nyekundu.
Wanawake wenye akili hawapendi kwa upofu hadi kufikia hatua ya kupuuza bendera nyekundu inayotoa tahadhari ya maisha yao.
#11 Hawavunji maadili au Imani yako kwa ajili ya Mwanamume.
Wanawake wenye akili wana maadili. Wana misingi ambayo wanaiheshimu sana, na hawako tayari kuharibu maadili au Imani yao kwa ajili ya mwanaume.
#12 Hawaachi jukumu lao la ngono mikononi mwa mwanamume..
Wanawake wenye akili wanaelewa kuwa kupata mtoto hubadilisha kabisa maisha yao, na hii inawaathiri zaidi wao kuliko mwanaume.
Wanaume hawapati mimba.
Kwa hivyo, wanawake wenye akili huwajibika ipasavyo kwa maisha yao ya ngono. Hawatajiweka katika hatari ya kupata mtoto kama hawana maandalizi ya malezi au kuzaa na mwanamume ambaye hayuko tayari kuwajibikia jukumu hilo la mtoto.
#13 Hawajiachi kutendewa kama takataka ili tu kubaki na mwanamume.
Wanawake wenye akili hawavumilii uhusiano unaowanyima amani ya moyo wao. Hawako tayari kuendelea na mahusiano ambayo wanadharauliwa, na hawathaminiwi.
Hawana maamuzi ya kusita sita kutembea mbali na uhusiano wenye sumu ambayo inaondoa furaha yao na kujithamini kwao.
#14. Hawapendi kijinga
Upendo ni upofu, kuna wakati sote tumefanya mambo ya kijinga kwa ajili ya mapenzi wakati fulani katika maisha yetu.
Lakini, wanawake wenye akili, wana busara ya kutosha hawawezi kuruhusu kupoteza mambo muhimu katika maisha yao kwa sababu ya kumpenda mwanaume.
Wanawake wenye akili hawaruhusu hisia zitawale maamuzi yao pasipo kuushirikisha ubongo wao.Hawajapofushwa na hisia. Ingawa wanapenda na kwa uaminifu, lakini wanapenda kwa akili.
#15 Hawaruhusu uhusiano au ukosefu wake kuwafafanua
Wanawake wenye busara hawaruhusu hali yao ya uhusiano kuwafafanua.Ndiyo, wanatamani kupenda na kupendwa tena.hata hivyo, hawaruhusu ukosefu wa upendo uharibu furaha yao.
#16 Hawamfanyi mwanaume kuwa mpango wao wa kifedha.
Wanawake wenye akili timamu wanaelewa kwamba “Ulinzi bora wa mwanamke ni pesa zake mwenyewe.” alisema Clare Boothe Luce.
Huwa hawaruhusu hatima yao ya kifedha iwe mikononi mwa mtu. Wanawake wenye akili huamini kuwa moja ya sababu kubwa ya baadhi ya wanawake wengi kunaswa katika mahusiano yasiyo na furaha na ndoa zenye maumivu, kudharauliwa, kutokuthaminiwa ni kutokana na utegemezi wa kifedha walionao kwa wanaume.
Utegemezi wako wa kifedha kwa mtu unadhibiti maisha yako katika kila eneo, unapokuwa na pesa zako mwenyewe, ni rahisi kufanya uchaguzi wako wako mwenyewe na utaweza kujitunza kila inapobidi pasipo kumtegemea Mwanaume.
Wanawake wenye akili hutafuta pesa zao wenyewe, hawamtegemei mwanaume.Chochote mwanamume anachowapa ni kama ni icing kwenye keki.
#17 Hawaruhusu mwanamume adharau familia yao na watu wanaowapenda.
Wanawake wenye akili timamu wanathamini familia zao na marafiki zao kama vile wanavyowathamini wanaume wao.
Hawaruhusu familia zao na marafiki zao kudharau mtu wao na hawaruhusu mwanamume wao kuwadharau wapendwa wao pia, Wana akili za kutosha kudumisha usawa huu
#18. Wanawake wenye akili mahusiano kwao sio kwa ajili ya kuchezeana kimwili peke yake.
Wanawake wenye akili wanajua kuwa umri wa usichana wao hauwasubiri, Hivyo mahusiano kwao sio kwa ajili ya kuchezeana tuu kimwili pasipo mipango, malengo, Wala maono yoyote yale ya baadae.
#19. Wanajikubali walivyo..
Wanawake wenye akili hujikubali walivyo, hawana muda wa kufake kwa kujiongezea mambo mengi ya bandia katika miili yao ili waonekane wakuvutia.
Huamini kuwa vile walivyo niwa kipekee sana.
#20. Wana hofu ya MUNGU…
Imeandikwa Wanawake ni jeshi kubwa, na ni ukweli usio pingika kuwa wanawake wana nguvu kubwa sana katika ulimwengu wa Kiroho.
Wanawake wenye akili hutumia fursa hii ipasavyo katika kuitafuata nguvu ambayo MWENYEZI-MUNGU kaiweka ndani yao. Kwa njia ya Ibaada, Sala, Maombi pamoja na usomaji wa Maandiko Matakatifu…
Humtanguliza MUNGU katika kila jambo, katika maisha yao.Hawapo tayari kuharibu uhusiano wao na MUNGU wa kiibaada kwa ajili ya mahusiano na mwanaume.
NB;- Haya ni mambo 20 ambayo wanawake wenye akili timamu hawafanyi kwa ajili ya mahusiano.
Kama mwanamke Ikiwa umekuwa ukifanya jambo lolote kati ya yaliyoorodheshwa, usijisikie vibaya.Mwanamke mwenye akili pia, ni yule ambaye yuko tayari kufanya mabadiliko anapotambua kile ambacho amekuwa akifanya vibaya.
Mwanamke asiye na akili timamu ni yule anayejaribu kutafuta njia za kupingana na ukweli ili aufanye uonekane kuwa ni uongo.
TUZIDI KUJIFUNZA NA TUSICHOKE KUJIFUNZA
Imeandaliwa na:-
Psychologist & Counselor,
Public speaker, Author
Spiritual mentor,
MWLSUNZU
0765900743(WhatsApp