Timu ya Kiyovu Sports ya Rwanda ipo katika wakati mgumu baada ya kukumbwa na wimbi la ukata wa fedha kitu ambacho kinaweza kusababisha kushindwa kushiriki katika mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Kombe la amani.
Mbali ya hivyo kumekuwa na kesi mbali mbali kuhusu matumizi mabaya ya madaraka ndani ya klabu hiyo na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Juvenal Mvukiyehe wakimshutumu kutumia fedha vibaya za klabu wakati wa uongozi wake.
Juvenal Mvukiyehe nae amepeleka mashitaka ndani ya Shirikisho la soka Rwanda Ferwafa akimshutumu kusema kuwa kiongozi wa sasa Jean François Régis Ndorimana amekuwa akimsemea uongo kuwa alikuwa anawaroga wachezaji wa klabu hiyo.
Kwa upande mwingine Mhazini Msaidizi wa klabu hiyo Abdulkarim Mbonyumuvunyi ameitwa na mamlaka ya kupambana na rushwa RIB kuhusu kumpatia hundi feki ya milioni 61 aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Juvenal Mvukiyehe.
Kwasasa Klabu hiyo,inakamata nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu Rwanda ikiwa na alama 21 katika michezo 15.