6: KENYA: Nairobi dabi (Mashemeji Derby)

KBC
Maelezo ya picha,Wanapokutana mashabiki wa AFC Leopards na Gor Mahia ni burudani ya utani mtaani mpaka nyumbani

Mechi kati ya A.F.C. LEOPARDS na GOR MAHIA F.C ilikuwa moja ya ‘dabi’ matata katika soka la Afrika Mashariki. Kwa sasa debi hii kidogo imepoteza mvuto kiasi kutokana na soka la Kenya kupitia misukosuko mingi ya rushwa, utawala na siasa.

Pamoja na hayo, panapokuwa na mchezo unaozikutanisha timu hizi, hamasa yake katika mitaa ya Kirinyaga, Tom Mboya, Naivasha, Baringo, Bibi wa Shafi na kwingineko inaendelea kuwa kubwa.

Gor Mahia maarufu kama Ko galo na Afc Leopards almaarufu Ingwe walikutana Jumapili ya Mei 8 katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani katika mchezo wa 94 kati ya mahasimu hao wa tangu ujadi uanze kati yao. Timu hizo zilienda sare ya 1-1 katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta. Dabi ya kwanza ilipigwa Mei 5 mwaka 1968. Awali mchezo huu ulitajwa kama debi ya Nairobi baadae ikapata umaarufu kwa jija la debi ya Mashemeji , kutokana na uhusiano wa karibu kifamilia na kitabaka kati ya Ingwe iliyo na wafuasi wengi wa asili ya Abaluhya na Gor iliyoa na idadi kubwa ya wafuasi kutoka koo ya Dholuo.

5. GHANA: Ghana Dabi

Utamu wa soka la Afrika Magharibi unajengwa na mechi za Dabi, moja ya debi kubwa afrika magharibi ni kati ya Hearts of Oak na Asante Kotoko. Ingawa kuna umbali wa kilometa karibu 248 kutoka Kumasi mpaka Accra zilipo klabu hizi, lakini ushindani wao unaleta aina tofauti ya hasama la soka Ghana na Afrika Magharibi.

Asante Kotoko inayotokea Kumasi, eneo la Ashanti, wakitumia uwanja wa nyumbani wa Baba Yara Stadium, Amakom, Kumasi wanaonekana kuwanyanyasa Hearts of Oak, kwa kutwa mataji 24 ya ligi kuu ya Ghana lakini katima michezo 26 iliyopita ya ligi ya nyambani iliyowahusisha watani hao wa jadi, Hearts imefanikiwa kushinda 8 dhidi ya 7 ya Asante, huku zikienda sare 9.

4. MOROCCO: Casablanca Dabi

Casablanca

Ni Dabi kati ya Wydad Casablanca na Raja Casablanca kutoka katika mji wa Casablanca ambo wanapokutana katika dimba maarufu la dabi hiyo la Stade Mohammed V ni mechi ya aina yake na yenye hadhi ya kimataifa. Kama ilivyo kwa Simba na Yanga nchini Tanzania, mashabiki wengi wa Morocco wana ushabiki na klabu hizi mbili. Mchezo wa kwanza kabisa kukutanisha timu hizi ulipigwa mwaka 1956 na tangu wakati huo Raja amekuwa mwiba zaidi kwa Wydad akishinda michezo 39 wakati Wydad amefanikiwa kushinda michezo 32.

3. TUNISIA: Tunis Dabi

Tunis Derby

Debi hii ni kati ya timu maarufu nchini Tunisia, Club Africain inayoonekana ni timu ya watu w akipato cha chini na Esperance de Tunis, inayotajwa kushabikiwa na ‘vibpopa’.

Hizi ni timu mahasimu wakubwa nchini humo, ambazo zinalinganishwa na Dabi ya Milan kati ya Ac Milan na Inter Milan kwa sababu ya kutumia uwanja wa nyumbani mmoja.

Mahasimu hawa wanatumia uwanja wa the Stade Olympique de Rades uliopo Tunis, kwa ajili ya mechi zao za nyumbani.

2. AFRIKA KUSINI: Soweto Dabi

Soweto Debi ya Afrika Kusini, inatajwa kuwa kama moja ya dabi maarufu barani Afrika, ikizihusisha klabu maarufu kutoka mji wa Soweto, Kaizer Chiefs na Orlando Pirates.

Ikiwa na makazi Soweto, Johannesburg, Kaizer Chiefs iliasisiwa na mchezaji wa zamani wa Orlando Pirates, Kaizer Motaung baada ya kutofautiana na viongozi wa juu wa Orlando kukiwa na uhusiano wa hatua yake ya kwenda kucheza soka Marekani, kwenye timu ya Atlanta Chiefs Mechi ya kwanza ya debi hii ilipigwa Januari 24, 1970 na uhasama ulichagizwa zaidi baada ya

1. MISRI: Cairo Dabi

Cairo
Maelezo ya picha,Rangi hizi za shangwe na hamasa hutawala sana zinapokutana Al ahly na Zamaleki mjini Cairo

Pengine hii ndiyo dabi maarufu zaidi Afrika, ikizihusisha klabu za kongwe na kubwa Afrika, Al ahly na Zamaleki. Vilabu vyote hivi vimetajwa na shirikisho la soka Africa kama miongoni mwa vilabu bora vya karne ya 20. Uhasama wa kisoka uliopo baina ya timu hizi mbili ni mkubwa, kiasi cha kujenga mpaka hofu ya kawaida kwa mchezaji kuhama kutoka timu timu moja kwenda timu nyingine kati ya hizi. Ni ngumu. Inaelezwa pia hii ndiyo dedi ya inayotazwa zaidi miongoni mwa debi za Afrika.

Inaweza ikawa kitu cha kufikirika Simba na Yanga kutazamwa nje ya Afrika achilia mbali Afrika Mashariki, mechi kati ya Al ahly na Zamaleki ni maarufu na inatazamwa pia katika nchi za Mashariki ya kati. Ni mechi ghali kuiandaa na kuitazama, inayohusisha timu ghali na wachezaji ghali Afrika. Katika michezo yote waliyokutana, Al Ahly imeonekana kufanya vyema ikishinda mara 105 Zamaleki ikishinda 58 na kwenda sare mara 79.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *