Dalili zinazo kuonyesha kuwa umepoteza au amepoteza hisia na wewe.

Dalili zinazo kuonyesha kuwa umepoteza au amepoteza hisia na wewe.

1️⃣ Tabia ya kulaumu.

〰️ Ukiona umeanza kumulaumu mwenzi wako kwa kila jambo baya linalotokea maishani mwako kwa kila atakachofanya, ni dalili inayoonyesha kuwa huna hisia nae tena tofauti na ilivyokuwa mwanzo..

2️⃣ Huna muda wa kufanya mazungumzo nae..

〰️ Ukiona huna muda wa kukaa na kufanya mazungumzo na mwenzi wako licha ya yeye kuomba nafasi hiyo mara kwa mara,ni dalili inayoonyesha umepoteza hisia na mwenzi wako…

3️⃣ Hujali kuhusu mwenzi wako…

〰️ Unapoona mwenzi wako hajali kuhusu wewe kwa jambo lolote lile tofauti na ilivyokuwa awali, ni dalili inayokuonyesha kuwa mwenzi wako kapoteza hisia na wewe, kuna jambo ambalo halipo sawa Kati yenu ndio maana ipo hivyo tofauti na ilivyokuwa awali.

4️⃣ Mabadiliko ya tabia.

〰️ Ikiwa mwenzi wako ameanza kuonyesha Mabadiliko ya kitabia ikiwemo kiburi, jeuri, usaliti wa waziwazi nakadhalika tofauti na ilivyokuwa awali. Hii ni dalili inayoonyesha kuwa Kuna mabadiliko ya kihisia kwake juu yako,yanayomfanya apoteze hisia na wewe..

5️⃣ Tabia ya kukuhumu.

〰️ Ikiwa unahukumiwa kwa kunyoshewa kidole kwa kila kinachotokea kuwa wewe ndio chanzo hata kama yeye ndio chanzo ni dalili inayoonyesha kapoteza hisia na wewe, Hivyo anajitahidi akufanye ujione wewe ndio mkosaji hata kwa makosa ambayo yeye ndio chanzo cha yote….

6️⃣ Amebadilika baada ya kupata kazi au wewe kupoteza au kufukuzwa kazi..

〰️ Ikiwa utagundua kuna Mabadiliko makubwa ya mwenzi wako yaliyochangiwa na yeye kupata kazi, kupandishwa cheo au kuhamishwa eneo la kazi. Au wewe kufukuzwa kazi, au kukoswa kazi tofauti na ilivyokuwa awali ni dalili inayokujulisha pia kapoteza hisia na wewe…

7️⃣ Mabadiliko ya tendo la Ndoa.

〰️ Tendo la ndoa ni muunganisho muhimu sana katika maisha ya ndoa, Ikiwa utagundua kuwa kuna Mabadiliko ya maisha ya tendo la ndoa tofauti na alivyokuwa awali, tafuta kujua ni nini tatizo, Dalili hii hukujulisha kuwa mwenzi wako kapoteza hisia na wewe

8️⃣ Mabadiliko ya kitanda au vyumba.

〰️ Kama wanandoa mnapogundua Hali hii imejitokeza katika maisha ya ndoa ni dalili inayojulisha kuwa kuna hali ya kupotea kwa hisia kati yenu ndio maana mmefikishana katika hatua hii ya kutenganisha vitanda vya Kulala kila mmoja na chake, au kutengana kupitia vyumba vya Kulala….

9️⃣ Marafiki Ndio kipaumbele chako..

〰️ Kama mwanandoa unapofikia hatua ya Kuwapa kipaumbele marafiki zako tofauti na unavyopaswa kufanya kwa mwenzi wako, ni dalili inayoonyesha kuwa umepoteza hisia na mwenzi wako, Kuna Jambo halipo sawa linahitaji suluhisho haraka iwezekanavyo Kati yenu.

Unapofikia hatua ya kumuongea mwenzi wako kwa marafiki zako hasa kuongea madhaifu yake, Mambo mnayopaswa kuyajadili kama wanandoa tena chumbani huelezea ni kwa namna gani ulivyopteza hisia zako kwa mwenzi wako…

Hitimisho….

Mahusiano yanaweza kuwa magumu wakati fulani na ni kawaida kwa mahusiano kubadilika kadiri muda unavyopita. Na Mabadiliko hayo yanaweza kuwa ni pamoja na kupoteza hisia kwa mwenzi wako…

Ikiwa unapitia hali hii kwa sasa na huna uhakika wa hatima ya mahusiano yako, ni muhimu kukumbuka kuwa mahusiano yanaweza kupitia nyakati tofauti kama yasemavyo Maandiko Matakatifu…

Wakati wa kucheka na wakati wa kulia.

Wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia…

Wakati wa vita na wakati wa amani…

Wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga.

( Mhubiri Sura ya 3 )

Hali yako ya kujihisi umepoteza hisia na mwenzi wako, haimaanishi kwamba huwezi kuzipata tena. Katika kushughulikia urejesheshaji wa hisia zako kwa mwenzi wako Ikiwa utazingatia baadhi ya mambo yafutayo huwenda yakaleta matokeo chanya Katika mahusiano yako:-

〰️Tafuta kujua ni nini chanzo cha wewe au mwenzi wako kupoteza hisia..

〰️Tafuta kujua ni mabadiliko gani yaliyojitokeza yaliyopelekea kupotea kwa hisia kwako au kwa mwenzi wako.

〰️Jikumbushe kuhusu mazuri ya mwenzi wako…

〰️ Tafuta nafasi ya mazungumzo na mwenzi wako, zungumzeni kuhusu Mabadiliko ya hisia Kati yenu…

Ikiwa una nia ya kujaribu kufufua hisia za uhusiano wako kwa mwenzi wako,Jambo muhimu zaidi ni wote muwe na nia moja ya kujenga, haijalishi nyuma kulikuwa na mpasuko wa kutokuelewana kiasi gani, Ikiwa mtakaa chini kwa pamoja na kuzungumza kuhusu mpasuko wenu, Kuna uwezekano mkubwa wa kujenga nasio kubomoa mahusiano yenu.,

Ikiwa mmoja wenu hataki kujenga yawezekana kuna sabababu zinazokosa suluhisho anazozisimamia, zinazomsukuma kufanya maamuzi ya kutokuendelea na mahusiano Tena….

Kabla ya kufanya maamuzi kuachana na mwenzi wako, yanayotokana na kupotea kwa hisia zako kwa mwenzi wako ni muhimu pia kupata msaada wa Kisaikolojia ( Tiba ya mazungumzo ) Huwenda matibabu haya yakakupa ufahamu mkubwa katika ufanyikaji wa maamuzi yako, ili usije jutia maamuzi yako hapo baadae..

NB:- MUNGU hafurahishwi na kuachana, Mshukuru MUNGU wakati wa Furaha, kicheko na amani ya Ndoa yako…

Mshukuru na mkabidhi MUNGU pia wakati wa huzuni yako, maumivu yako, changamoto zako, Pamoja na mpasuko Katika ndoa yako. Atatenda!.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *