DALILI 8 AMBAZO NDOA YAKO INAKUFANYA UWE NA HUZUNI…

Katika maisha yako ya ndoa huzuni inaweza kuwa ni matokeo ya sababu kadhaa. Hakuna sababu moja ya uhakikia ya kujua kwamba ndoa yako inakufanya uwe na huzuni. Hata Hivyo, zituatazo ni baadhi ya dalili zazochangia huzuni katika maisha ya ndoa..

1. Mabishano ya mara kwa mara.

〰️ Mabishano na mizozo ya mara kwa mara yanayochangiwa na Kukosekana kwa mazungumzo sahihi yenye kusikilizana na kuelewana kwa pamoja ni miongoni mwa dalili inayochangia huzuni katika maisha ya ndoa. Lakini pia mabishano na mizozo ya mara kwa mara huzaa dharaulina katika maisha ya ndoa.

2. Ukosefu wa juhudi kutoka kwa mwenzi wako..

〰️ “Nimevunjika moyo Sana,najiona mpweke katika ndoa yangu”. Mawazo kama haya huzunguka katika akili yako na yatakufanya uhuzunike zaidi Ikiwa utajiona kuwa wewe ndio unaweka juhudi zaidi katika mahusiano yenu kuliko mwenzi wako.

3. Kukosekana kwa ukaribu..

〰️ Kinachowaweka wanandoa pamoja ni tamaa ya kukaa karibu na kila mmoja, kimwili, kiakili na kihisia. kando na kufanya mapenzi, kuna njia nyingi za kudumisha Uhusiano kati yako na mwenzi wako.
Njia hizi zinaweza kujumuisha kushikana mikono, kumbusu kabla ya kuondoka nyumbani, kununua zawadi na kadhalika. Vitendo vya ukaribu vinapokosekana katika maisha ya ndoa huchangia maisha ya huzuni katika ndoa…

4. Ukosefu wa tendo la ndoa..

〰️ Tendo la ndoa ni muunganisho wa ndoa, Ikiwa tendo hili litakosekana litaibua ugomvi utakaopelekea huzuni katika maisha ya ndoa kwa wanandoa…

5. Maisha ya kinyongo..

〰️ Matatizo, ugomvi na migogoro isiyopatiwa ufumbuzi kupitia mazungumzo huwa chanzo cha kuhifadhi chuki pamoja na hasira katika maisha ya ndoa.Hali hii hupelekea maisha ya huzuni katika ndoa kwa wanandoa.

6. Kutajwa kwa talaka

〰️ Kutajwa kwa talaka katika ndoa inaweza kuwa chanzo Cha huzuni kwa mume au mke, Ikiwa mwenzi wako kila ugomvi unapotokea anapendekeza muachane kwa kupeana talaka badala ya kutafuta nini chanzo Cha tatizo na suluhisho la tatizo, Hali hii inaweza kuwa ni sababu inayokuvunja moyo na kukufanya uishi katika maisha yasiyokuwa na furaha katika ndoa yako…

7. Kutokushirikishana katika kufanya maamuzi..

〰️ Ndoa ni muunganiko wa kimwili,kiakili, kihisia na kiroho. Kukosekana kwa Ushirikiano hasa katika kufanya maamuzi kwa kushirikishana huwa chanzo Cha msongo wa mawazo kwa pande moja hasa isiyoshirikishwa katika mchakato wa kufanya maamuzi ya kifamilia.

8. Kupoteza hisia….

Chumba cha kulala ni mahali ambapo wanandoa wengi hutatua tofauti zao. Ikiwa katika Wakati wa usiku umekuwa ukitafuta visingizio vya kutokwenda kulala au kuchelewa kulala, au wakati mwingine mnalala mmeweka m paka wa blanket katikati yenu, kila mmoja kitanda chake, au chumba chake, dalili hii huonyesha kuwa kati ya wanandoa kuna mmoja amepoteza hisia na mwenzi wake hali hii hupelekea maisha ya huzuni kwa mwanandoa au wanandoa…..

TUZIDI KUJIFUNZA NA TUSICHOKE KUJIFUNZA ✍️

Huduma ya saikolojia na ushauri nasihi kwa Matatizo ya mahusiano ( urafiki, Uchumba, ndoa) Inapatikana…..

Karibu tukuhudumie, kwa maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa huduma piga simu namba:-
0765900743/0717221610

Msaikolojia na mshauri nasihi,
Mwlsunzu 

See less

Comments

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *