Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC imefuta matokeo katika baadhi ya maeneo kutokana na kukiukwa kwa kanuni za Uchaguzi.
Mbali ya hayo CENI imesema kumeonekana viashria vya wizi wa kura na usalama mdogo na kusababisha tume hiyo kuyafuta matokeo.
Ushindi wa wabunge 80 kutoka maeneo ya Kwilu,Yokama,Ubangi na Equateur umefutwa mpaka pale hatua nyingine zitakapochukuliwa.
CENI imesema kuwa uchunguzi unaendelea kufanyika kwa baadhi ya maafisa wake kuhusika katika wizi huo wa kura na atakayebainika sheria itafuata mkondo wake.
Pia tume hiyo inaendelea kusikiliza rufaa ya aliyekuwa mgombea wa Urais Theodore Ngoy katika uchaguzi uliofanyika Desemba 20,2023 uliomuweka madarakani Felix Tshisekedi kwa muhula wa pili mfululizo.