AINA nne ZA WAPENZI KATIKA MAHUSIANO kabla ya ndoa

Katika mahusiano watu wengi tumeumizwa na kujutia maisha yetu baada ya kutendwa na wale tuliodhania kuwa ni watu sahihi na wa karibu kwetu, kumbe walikuwa siyo watu wazuri Kama tulivyowadhania.

Leo nakushirikisha aina nne za Wapenzi na tabia zao katika Mahusiano.

1. Mpenzi wa Kweli.

2. Mpenzi Mnafiki.

3. Mpenzi Mnyonyaji.

4. Mpenzi Mpoteza muda.

1️⃣ MPENZI WA KWELI:-

〰️Aina hii ya Mpenzi furaha yake ni kukuona:- Unachangamka,Una amani,

Unafanikiwa, Umestawi, Una afya njema

Unafaulu katika kila unachokifanya,

Mambo yako yanaenda vizuri.

〰️Ni Yule :

• Anayekujali kwa kila hali,

• Anayekujulia hali muda mwingi,

• Anakuthamini ,

• Anakuonyesha upendo wa dhati kwa vitendo si kwa maneno tu.

• Anakushirikisha mambo yake.

• Ni mkweli na mwaminifu kwako.

• Anatafuta mbinu za kukufanya ufurahi,utabasamu,ucheke na uwe na amani.

• Ndiye mfariji na mdhamini wako wa kwanza unapopatwa na magumu.

• Anakuheshimu na kuheshimu mawazo ,maoni na mapendekezo yako.

• Hawezi kukusema vibaya na Hataki kusikia ukisemwa na watu vibaya hata kidogo badala yake anakutetea.

• Ni mwaminifu katika mambo yote.

• Siku zote anatafuta maslahi ya ninyi wote (wewe na yeye) ,

• Akiwa nacho anakukumbuka,asipokuwa nacho anakupa taarifa

• Ni mwepesi wa kukuomba msamaha,

• Anakuomba ushauri,

• Mara zote anakupa nafasi ya kutoa mapendekezo,mawazo na maoni yako kuhusu jambo lolote linalowahusu.

• Mnapopishana kwa jambo lolote anajitahidi kutafuta suluhu haraka iwezekanavyo ili myamalize.

2️⃣ MPENZI MNAFIKI.

Sifa za Mpenzi mnafiki.

〰️Anajidai kukupenda anapokuona lakini mnapoachana anakusahau na hana mpango na wewe,

Usipombipu,kumtumia meseji au kumpigia simu,hakutafuti wala kukujulia hali.

〰️Anakupigia simu pindi anapokuwa na shida na wewe au anapohitaji faraja kutoka kwako.

〰️ Anakuinjoyi mara nyingi na kujidai kukupenda kwa dhati pasipo kuwa na ukweli wowote.

〰️Ana maneno mengi ya udanganyifu.

〰️Ni mtoa ahadi nyingi asizotekeleza, na Hana upendo wa dhati na wewe hata kidogo

〰️Anakusengenya ,kukushusha hadhi na kukubeza anapokuwa na watu wengine.

〰️Hapendi mafanikio yako.

〰️Siyo mwaminifu hata kidogo.

〰️Anatafuta visingizo na namna ya kukuacha.

3️⃣ MPENZI MNYONYAJI.

Sifa zake.

〰️Anatafuta faida kutoka kwako,anahitaji kunufaika kupitia wewe kwa namna moja ama nyingine .

〰️Ana agenda ya siri kuhusu wewe, upendo wake kwako ni pesa tuu.

〰️Anakuwa karibu sana na wewe ili umpe kile anachohitaji: Mfano: PESA, MWILI WAKO, AJIRA,(n.K) akishafanikiwa kupata kile alichokihitaji anakusahau kabisa na wala hataki kukuona na anabadili hata namba za simu .

〰️Si mwepesi kukuomba msamaha anapokukosea baada ya kupata kile alichokuwa anahitaji kutoka kwako.

〰️Hakubembelezi hata kidogo baada ya kupata kile alichokitaka kwako. Kuna wakati anaweza kuwa mkali kwako.

〰️ Msimamo wake siku zote ni “POTELEA MBALI”

〰️Mara zote anakuwekea masharti katika Mahusiano yenu, yenye lengo la kupata kile anachokitaka kutoka kwako.

〰️ Anapotaka kukuacha anatafuta sababu isiyo ya msingi yaani atatafuta kisingizio.

〰️Haoni aibu kukuomba vitu mbalimbali kama vile Pesa , Mali, Mwili wako nk…

4️⃣ MPENZI MPOTEZA MUDA.

Sifa zake:–

〰️ Anatoa ahadi kibao kwa asilimia kubwa sana lakini hatekelezi.

〰️ Anakukatisha tamaa unapotaka kufanya jambo linaloleta maendeleo.

〰️ Hakutii moyo hata siku moja.

〰️ Anakuthibitishia kwamba huwezi kabisa kufanya kama wengine wanavyofanya.

〰️Anakucheleweshea mipango yako na ratiba zako.

〰️Anakuahidi kuwa mko pamoja sana, lakini anakupotezea muda tena kwa makusudi.

〰️ Ana wivu wa kijinga jinga usiyokuwa na sababu za msingi.

〰️Anakuvurugia mipango na ratiba zako.

〰️ Anakuwekea masharti mengi katika uhusiano wenu.

〰️ Anajali maslahi yake binafsi ,haangalii maslahi yako.

〰️ Amejaa maeneno ya uwongo na udanganyifu.

〰️ Haoni fursa,na wala hajishughulishi kwa mambo yanayowahusu.

〰️Hana maono wala mipango inayohusu maendeleo yenu na hatima yenu baadaye.

〰️Anakuongezea msongo wa mawazo siku hadi siku kwa maneno yasiyokuwa ya kukujenga.

〰️ Haongei mambo ya msingi na hana pointi za msingi katika Mazungumzo yenu.

〰️ Anapenda mpoteze muda mwingi kwenye vitu visivyokuwa na tija kama vile starehe, michezo na burudani nk….

NB:-

Natumai kupitia Aina hizi 4 umejifunza na huwenda umejua mpenzi wako ni Aina gani kwako…..

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *