AINA 10 ZA WANAWAKE NA TABIA ZAO

*AINA 10 ZA WANAWAKE NA TABIA ZAO* .

1️⃣ *Mommy Types* .

〰️ Ni Aina ya wasichana au wanawake ambao huonyesha tabia ya umama. Hupenda kujali kupita kiasi. Mfano katika mahusiano usipomtumia ujumbe wa kufika sehemu uliyomwambia unaenda tarajia kupokea simu zisizopungua 10.

2️⃣. *The Listener* .

〰️ Ni Aina ya wasichana au wanawake inayopendwa na wanaume wengi zaidi Duniani. wapole wenye nidhamu, wanyenyekevu na huonekana kujali Sana. Huwa niwasikilizaji bila kuhukumu au kuwa na usumbufu wowote katika mazungumzo yao.

Katika mahusiano huonekana niwa kimya sana ikiwa hawatapewa nafasi ya kuzungumza, na niwatunzaji wa matukio. Siku ukitokea ugomvi na akapata nafasi ya kuongea atapanga mtiririko wa matukio yote uliyomfanyia na ikiwa ugomvi ni mkubwa, wako tayari kuvunja mahusiano au kufanya Jambo lolote baya

3️⃣. *Superwomen* .

〰️Ni Aina ya wasichana au wanawake ambayo huwa ni wagumu kwa asili yao. Vipaumbele vyao wakati wote huwa ni malengo yao. Wanafanya kazi kwa bidii. Na huwa ni wagumu Sana kukueleza kile wanachopitia. Hupenda Sana kuungwa mkono maamuzi yao. Hawapendi kuhukumiwa au kutiliwa mashaka. Wanapenda kujitegemea Zaidi.

Huwa na mihemko Sana katika ufanyaji wa mambo yao hali inayowafanya kukoswa utulivu, Huficha hisia zao.

Ikiwa umepata mtu wa aina hii katika mahusiano unahitajika kuwa mwangalifu sana juu ya matendo yao, kwa Sababu Haijalishi ana nguvu kiasi gani, wao wanahitaji mtu wa kuwaangalia Sana.

4️⃣ *Ms. Perfectionist*

〰️ Ni aina ya wasichana au wanawake wanaopenda kufanya mambo yao kwa uzuri na umakini mkubwa. Wanapenda kutii kanuni na taratibu kulingana na mazingira waliyopo. Niwenye nidhamu, hupenda usafi na kupangilia vitu vyao katika ubora. Hawapendi kukosolewa, hupenda kusapotiwa na kusifiwa katika kila kitu wanachokifanya.

Katika mahusiano huwa ni wazuri ikiwa utaendana nao, lakini huwa niwasumbufu ikiwa utakuwa kinyume nao.

5️⃣. *Panda girl’s*

〰️ Ni aina ya wasichana au wanawake ambao huwa wavivu sana. Hupenda maisha ya starehe yasiyochosha miili yao. Hupenda kufanyiwa kila kitu. Ni ving’ang’anizi sana ikiwa watataka kitu wanapenda wakipate kwa huohuo mda.

Katika mahusiano hupenda maisha ya bata sana, na niwasumbufu hupenda kila mda waoonekane usoni mwa mwanaume waliyenaye katika mahusiano. Ikiwa huna tv Basi wao ndoo huoonekana Kama video mbele yako.

Ni aina ya wanawake ambao wanauwezo wa kumtengenezea mwanaume Ratiba ya maisha yake kutokana na mihemko yao.

6️⃣. *Boss lady*

〰️ Nia Aina ya wanawake hodari, huru na wasioogopa kusema Mawazo yao. Wana ndoto Kubwa ni waongeaji na hupenda kutetea haki zao. Ni wanawake wenye ujuzi na huonekana jasiri kupitia mafanikio yao. waaminifu, hupenda mamlaka, na hupenda kujitegemea.

Katika mahusiano Hupenda kumiliki na kuongoza kila kitu. Wanapenda kuongoza kwani hujiona ni wenye mamlaka.Huwa hawana hofu huamini wanaume na wanawake Wana uwezo sawa wa kuongoza na kunyakua kila fursa.

Hawapendi Kushughulikiwa kama watu wa kawaida ( wabinafsi Sana)

Huwa wanajua nafasi zao ziko juu hivyo watakupiga vita ikiwa utaingilia malengo yao.

7️⃣. *Drama Queen* .

〰️Ni Aina ya wasichana au wanawake ambao hupenda kuzidisha hali walizopewa iwe ni katika maumbile yao au katika maisha yao ya kila siku. Hupenda kucopy sana kila kitu, mwonekano wao umejaa edit nyingi sana, Kila wanachokiona kinachohusu mwonekano wao wanataka wae nacho,huwa sio wabunifu.Wanapenda kujaliwa sana na hupenda kuwa tegemezi hata kama wanaweza kujitegemea wao wenyewe.

Katika mahusiano huwa ni kinyume Cha panda girls, wanapenda mda wao mwingi wawe chini ya uangalizi wa mwanaume. Huwa hawapendi waume zao waonekana na wanawake wengine hata Kama awe ni rafiki wa kawaida. Wana wivu mkubwa Sana katika mahusiano.

8️⃣. *The Nerd* .

〰️ Ni aina ya wanawake wenye akili, wenye ufahamua na wanaojifunza mambo mbalimbali. Hupenda maisha yao binafsi hawapendi maisha ya kuigiza. Huwa ni wenye malengo wanayoyatamani kuyafikia, katika mahusiano utapata wakati wao ikiwa watamaliza masomo yao au kufikia malengo yao. Ni wenye ushawishi mkubwa na ni wenye marafiki wengi.

Hawapendi kusifiwa na kuonekana Tofauti na wanawake Wengine, hupenda kuonekana wenye ukawaida.

9️⃣. *The guy’s girls* .

〰️Ni aina ya wasichana au wanawake ambao hupenda zaidi ushirika na wanaume. Hupendelea kufanya mambo ya kiume na wakati mwingine huonekana katika mwonekano wa uanaume. Huwa Ni wenye malengo na mipango mikubwa Sana. Huwa ni wenye nguvu ya Ushawishi ikiwa atakuwa na Jambo lake lazima atahakikisha linafanyika.

Huonekana kuwa niwenye ndoto Kubwa kupitia Mawazo yao. Katika mahusiano ni marachache kutazama urafiki wake na wanaume katika mambo ya kimapenzi. Anaweza kuwa na mpenzi ambaye wanashiriki nae Mara moja na kwa wakati..wanajulikana pia kama Tom-boy.

1️⃣0️⃣. *The Fashionista* .

〰️ Ni aina ya wanawake ambao niwabunifu sana na wanamitindo.

Huonekana vizuri wakati wote, Kama sio kumpenda basi lazima utamtamani tuu wakati utakapokutana nae.

Wanajua bidhaa gani ni toleo jipya.

Mavazi yake yaweza kuwa niya bei rahisi lakini ni wanawake wanaojua kupangilia Sana.Ni wanawake wenye mizunguko sana, wanapenda kusafiri na hupendelea kuonekana katika kila sherehe.

Tuzidi kujifunza, Tusichoke kujifunza.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *